Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Victoria Mwanziva L, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maji- Wilaya ya Lindi na kubainisha mafanikio na mageuzi makubwa Sekta ya Maji ikiwa ni kazi kubwa iliofanya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Katika ziara hiyo DC Mwanziva ameambatana na Watendaji wa wilaya ya Lindi wakiongozwa na Kaimu Meneja wa Wilaya ya RUWASA Lindi Mhandisi Athanas Lume
Ziara hii imetanabaisha kuwa Katika kipindi cha miaka 4 (Machi, 2021 hadi Disemba, 2024) Rais Samia ametoa kiasi cha shilingi bilioni kitanzania 5.71 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 17 jimbo la Mchinga na Shilingi 12.79 billioni kwa ajili ya ya utekelezaji wa miradi 13 katika Halmashauri ya Mtama ikiwemo miradi 5 ya uchimbaji wa visima katika kila jimbo la uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa Zaidi ya asilimia 85 ya wananchi waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama.
DC Mwanziva amesema Magari ya Uchimbaji Visima aliyonunua Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yenye adhma uchimbaji wa visima mia 900 vya maji katika kila Mkoa yanafanya kazi na visima hivyo vinachimbwa Ili wananchi waweze kurahisishiwa kupata maji yaliyo safi na salama, Mkuu wa Wilaya ya Lindi amekagua zoezi la uchimbaji wa Visima ambalo limekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.