
Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza dhamira ya serikali kujenga jamii jumuishi, yenye haki na usawa wa kijinsia.
Rais Samia ameeleza hayo kwwnyw maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha yakihudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka sekta mbalimbali za uchumi.
Rais Dkt. Samia ameeleza hatua muhimu ambazo Tanzania imepiga katika kufanikisha malengo ya azimio la Beijing la 1995 na Dira ya Maendeleo Endelevu.
Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kupambana na mila kandamizi na kuhakikisha kila msichana na mwanamke anapata fursa sawa kufanikisha ndoto zake.
Aidha, amehimiza uwekezaji kwa vijana ili kuimarisha harakati za usawa wa kijinsia kwa vizazi vijavyo.