
Wizara ya Fedha inaendelea na zoezi la utoaji wa elimu ya fedha katika maeneo mbalimbali ambapo mpaka sasa wameshaifikia mikoa 15, ukiwemo mkoa wa Kagera, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Pwani, Morogoro, Rukwa, Lindi, Mtwara, Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mara.
Hata hivyo wizara ya Fedha inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi yote ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2021/2022 hadi 2029/2930 ambapo malengo ni kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na elimu hiyo ifikapo mwaka 2026.
Katika zoezi la utoaji elimu ya fedha Wizara ya Fedha, imeambatana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC.