Back to top

RAIS SAMIA AKEMEA UDANGANYIFU, WIZI NA UPINDISHAJI HAKI

17 March 2025
Share

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka waratibu wa mfuko wa fidia ya ardhi kubadilika, katika kutimiza majukumu yao ya kila siku, akikemea tabia ya udanganyifu, wizi, na upindishaji wa haki katika ulipaji wa fidia kunakofanywa na baadhi ya watumishi.

Rais Samia ameeleza kuwa kumekuwa na malalamilo mengi kwa watendaji hao wakilalamimikiwa kwa kuwa na makandokando kwenye michakato ya fidia, wakati wa ufanyaji wa tathimin, sambamba na ucheleweshaji mkubwa wa fidia na ulipaji pungufu (mapunjo).

Rais Samia ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, wakati akizindua sera ya ardhi ya Mwaka 1995, toleo la mwaka 2023, akisema sera hiyo pamoja na mambo mengine itaimarisha mfuko wa fidia ya ardhi, kurahisisha ulipaji wa fidia kwa haki na kwa thamani halisi, ikidhibiti pia udanganyifu kupitia teknolojia.