
Wafugaji wametakiwa kufuata taratibu za ufugaji na malisho sahihi ya mifugo yao ili kupata mazao mazuri ya nyama, kwani kufanya hivyo kutaongeza soko la biashara hiyo ya mazao ya nyama ndani na nje ya nchi.
Afisa Mifugo Golden Festo Nzalallilam ameeleza haya mkoani Tanga, kuhusu elimu ya ufugaji bora katika kunenepesha mifugo, ili kupata mazao bora ya nyama Mkoani Tanga katika Wilaya ya Handen Kijiji cha Msomera.
Festo amewasisitiza wafugaji kuwa ni vyema wakafanya ufugaji wa kisasa ambao matokeo yake ni mazuri kibiashara, na kuwaambia wananchi wa Msomera kuwa eneo hilo kwa ufugaji na malisho ni zuri, hivyo anaimani mazao ya nyama yatakuwa bora na kuwafutia walaji wa nyama kutoka Msomera.