Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar wamefanikwa kukamata Shehena ya Magaloni 740 ya mafuta ya Kula ambayo yalikuwa yasafirishwe kwenda nje ya Zanzibar baada ya kubadilishwa nembo ya awali na kuwekwa nembo ya Oki.
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar-ZFDA-imefanikiwa kunasa shehena ya magaloni 740 ya mafuta ya kula yaliyokuwa yasafirishwe nje ya Zanzibar baada ya kubadilshwa nembo yake halisi na kuwekwa nembo ya Oki,magaloni hayo 740 yalikuwa yamehifadhiwa ndani ya tawi la CCM makadara Zanzibar.
Akizumgumza na vyombo vya habari katika eneo la operesheni hiyo makadara mjini Unguja ambapo magaloni hayo yalikuwa yakigeuzwa nembo za asili ndani ya tawi hilo la CCM Makadara kaimu mkurugenzi mtendaji wa wakala huo Dkt. Khamis Ali Omar amesema walipata taarifa na kuvamia eneo hilo wakati wa usiku na kukuta shehena hiyo huku mmiliki huyo akitoweka na anatafutwa ,mtendaji huyo amethibitisha kuwa mafuta ijayo yenye nembo ya Turkey yatoka Indonesia .
Kuonekana kwa mafuta hayo ndani ya tawi la CCM ilizua mjadala mkubwa na hofu ya tawi hilo kuhusika hata hivyo akiongea kwa simu naibu katibu mkuu CCM Dkt. Abdulah Juma Mabodi amekanusha CCM kuhusika kauli ambayo iliungwa mkono na katibu wa CCM jimbo la Malindi Salum Juma Ali aliyefika kwenye tukio hilo,huku mwakilishi wa kampuni hiyo ya Oki Zanzibar Salum Humud wa Sub Sahara amesema ni mtindo ambao lazima upigwe vita na serikali.
Wakti zoezi la kutaka kuyaondosha mafuta hayo likianza mmoja ya mtu anayetuhumiwa kuhusika na zoezi hilo aliibuka na kudai yeye hajui chochote n awalikuwawnatumiaeneo hulo kuhifadhi ndai ya tawi la ccm.