Back to top

Asilimia 43 ya watoto wamethiriwa na kichocho Kigoma.

06 July 2018
Share

Mkuu wa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Mwanamvua Mlindoko amesema asilimia 43 ya watoto wanaoishi katika vijiji vya mwambao katika Ziwa Tanganyika na katika wilaya za Buhigwe,Kasulu na Kibondo wana vimelea vya ugonjwa wa kichocho.

Amesema katika kijiji cha Mwakizega wilayani Uvinza wakati zoezi la utoaji dawa kwa watoto likiendelea ,kuwa utafiti uliofanywa na wizara ya afya umebaini ongezeko la magonjwa ya kichocho na minyoo tumbo hali ambayo imepelekea serikali kutoa tiba kinga kwa watoto wote zaidi ya laki tano wenye umri wa miaka mitano hadi 14 katika mkoa wa kigoma ili kuwakinga na magonjwa hayo.

 Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa Dk. Fadhil Kibaya amesema magonjwa yasiyopewa kipaumbele ambayo ni kichocho,pumu,minyoo,tauni, matende na ngiri maji yamekuwa yakisababisha vifo, ulemavu, maumivu ya muda mrefu na umaskini na kwamba kutolewa kwa dawa tiba kinga kutasaidia kutokomeza magonjwa hayo.