Rais John Pombe Magufuli ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Nyerere kupokea ndege mpya aina ya Boeing 787- 8 Dreamliner kutoka Marekan ambayo imeagizwa na serikali ya awamu ya tano.
Ndege hiyo kubwa ambayo imetengenezwa nchini Marekan imefika Majira ya saa kumi na na kupokelewa na Rais Magufuli na viongozi mbalimbali wa serikali na vyombo vya dola na wa kidini ambapo Rais Magufuli amesema kuwa hiyo imechangiwa na mchango wa mkubwa wa watanzania katika kuchangia kodi.
Akiongea baada ya kufanya ishara ya kuzindua ndege hiyo Rais Magufuli amesema kuwa ujio wa ndege hiyo utafungua mlango na kuongeza tija katika ukuaji wa uchumi na sekta ya usafirishaji na utalii na kilimo.
Kwa upande wa sekta binafsi ambayo imewakilishwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni mwenyekiti wa IPP Dakta Reginald Mengi ambaye amesema kwa mambo yanayofanywa na Rais ni vyema watanzania wakaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano.
Watu mbalimbali ambao wamejitokeza katik uwanja wa JK Nyerere wamepongeza ujio wa ndege yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 240.
Ndege ya Boeing 787 - 8 ni ya nne kununuliwa na serikali tangu kuingia kwa awamu ya tano chini Rais John Pombe Magufuli ikiwa ni katika kulifufua shirika la ndege nchini ATCL.