![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/Tunduru%2001.jpg?itok=O8ZQszWa)
Wananchi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wamelalamikia ubovu wa stendi ya wilaya hiyo ambapo imekuwa na mashimo na mawe hali inayoharibu magari hivyo wameiomba serikali kuitengeneza stendi hiyo.
Wakizungumza na ITV katika stendi hiyo ya mabasi yaendayo wilayani na mikoani wamesema kutokana na kukua kwa mji wa Tunduru stendi hiyo inahitajika marekebisho makubwa na kwamba wamekuwa wakiharibu magari yao kutokana ubovu wa stendi hiyo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera amesema kuwa serikali iko katika mchakato wa kujenga stendi nyingine ya kisasa itakayoendana na mji wa Tunduru kwa sasa.