Back to top

Mji wa Mikindani mkoani Mtwara watajwa kuwa kitovu cha utalii.

03 August 2018
Share

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga amewaagiza watumishi wawili wa idara ya mali kale waliopo kwenye mji wa kihistoria wa Mikindani mkoani Mtwara, kuandika andiko na kutuma kwa wadau mbalimbali ili kupata fedha za kukarabati majengo ya kale ya mji huo, huku akiutaja mji huo kuwa kitovu cha utalii mikoa ya Kusini.

Naibu Waziri Hasunga amesema hayo alipokutana na kamati ya ushauri kuhusu uhifadhi wa mji wa Mikindani ya TRADE AID na kubadilishana Mawazo na kisha kupata fursa ya kutembelea baadhi ya majengo ya kale ambapo amesema serikali haiwezi bila kuwashirikisha wadau katika ukarabati wa majengo hayo muhimu kwa taifa na kuonya migongano haitasaidia kuinua utalii mikoa ya Kusini. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amemshkuru Rais John Pombe Magufuli kwa mkazo wake wa kuimarisha utalii mikoa ya Kusini, kwani imewatia moyo katika kuhakikisha mali kale katika mkoa wa Mtwara zinatunzwa.