Back to top

Serikali yaagiza taka kusombwa usiku jijini Dar es Salaam.

10 September 2018
Share

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Paul Makonda ameyaagiza makampuni yaliyopata kandarasi wa kusomba taka jijini kufanyakazi usiku ili kuondokana na changamoto ya foleni na kuleta ufanisi utakaosaidia kufikia malengo ya kampeni ya kuliweka jiji la Dar es Salaam katika hali ya usafi.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau wa kampeni ya usafi jijini, Bwana Makonda amewataka wakandarasi hao kutumia muda huo ili kusombataka kwa wakati ikiwemo kuondoa michanga kwenye barabara zilizo na lami. 

Bwana Abubakari Kunenge ni katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kampeni ya usafi inalenga kusaidia kupunguza gharama za maisha kwa wakazi kwa kuondoa uwezekano wa kupata maradhi yanayoweza kuepukika ikiwemo kipindipindu.

Wakizungumzia kampeni ya usafi, baadhi ya wawakilishi wa taasisi wamepongeza maamuzi ya serikali ya kusomba taka usiku ili kuondokana na changamoto mbalimbali, huku wengine wakitaka vyombo vya habari kuongeza kasi zaidi ya kuhamisisha wananchi.