Back to top

Wafanyabiashara soko la mlango mmoja mwanza wamegoma

21 November 2018
Share

Wafanyabiashara katika soko la Mlango Mmoja jijini Mwanza wamaelazimika kufungua milango wanayotumia kuingia ndani ya soko hilo baada ya Halmashauri ya jiji hilo kushindwa kuwapatia vibali vya ujenzi wa maduka yao 29 pamoja na vibanda 55 vilivyoteketea kwa moto September 29 mwaka huu na kuwasababishia hasara ya Shilingi milioni 580. Na hivyo kusababisha askari wa kikosi cha kutuliza ghafia wenye silaha za moto na mabomu ya machozi kuwaamuru kwa nguvu wafanyabiashara hao kufungua milango ya soko hilo.