Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla amesema Tanzania imefanikiwa kupata tuzo na kuibuka mshindi wa kwanza kwa nchi zenye vivutio zaidi duniani uliozingatia ubora wa vivutio vya asili nchini Urusi.
Waziri Kigwangalla amesema hayo jijini Dar es Salaam katika kikao kilichoshirikisha ujumbe kutoka nchi ya Urusi ambapo ushindani wa tuzo hizo ulifanyika huku Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt.Damas Ndumbaro akisema kuwa wamefanya mazungumzo na makampuni 500 ya utalii ya Uchina kwa nia ya kuleta watalii nchini na kujenga hoteli za kitalii kwenye hifadhi za taifa.