Back to top

Jamii ya Wahadzabe Singida yaomba kutengewa maeneo yenye kupata dawa.

25 December 2018
Share

Jamii ya Wahadzabe wanaoishi katika kijiji cha Mwangeza kitongoji cha Kipamba wilayani Mkalama wameiomba serikali ya mkoa wa Singida  kuwatengea maeneo yenye uoto wa asili kwa ajili ya  kupata dawa za mizizi na kufanya  matambiko ya kimila.
 
Jamii hiyo ya Wahadzabe wamesema hayo kwa Mbunge wa Iramba mashariki Mheshimiwa Allan Kiula kwenye sherehe maalumu ya kimila ya  kusherekea sikuku ya kuzaliwa yesu kristo  iliyofanyika chini ya mti na kuhudhuriwa na  jamii hiyo kwa kucheza ngoma za asili na nyimbo za dini.