Back to top

Wananchi zaidi ya 700 Moshi wakosa huduma ya maji kwa zaidi ya wiki.

13 January 2019
Share

Wananchi zaidi ya 700 wa vijiji viwili vya Koresa  na Uchira wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameendelea kukosa huduma ya maji kwa zaidi ya wiki moja kwa kile kinachodaiwa ni mvutano  baina ya bodi mbili za maji zinazohudumia wananchi hao.

Wananchi wa vijiji hivyo wamesema hali ni mbaya kutokana na wanawake kuhangaika na ndoo za maji  kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji  safi na salama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya jumuiya ya watumia  Uchira Bw.Lazaro Mfinanga  amekiri kuwapo  kwa tatizo hilo   ambalo anadai linasababishwa na bodi ya maji Kirua Kahe Mtiririko  kuhujumu jumuiya ya watumia maji Uchira hali ambayo inasababisha adha kubwa kwa wananchi.
 
ITV imefika katika ofisi ya maji Kirua Kahe Mtiririko na kukutana na Meneja wa bodi hiyo bw.Mambeya Mshana ambaye  amesema tatizo  la ukosefu wa maji katika vijiji hivyo  linasabaishwa na uharibifu wa miundombinu kwenye matanki yanayosambaza maji kwenye vijiji hivyo na kwamba tayari mafundi wameanza matengenezo.