Idara ya uhamiaji mkoani Singida ina washikilia wahamiaji haramu ishirini na mbili wakiwemo familia tatu zenye watoto kutoka nchi za Burudi ,Kenya na Somalia ,ambao walikuwa wakisafiri kwa basi kutoka Tabora kupitia mkoani Mbeya hadi nchi ya Malawi kwa ajili ya kutafuta maisha .
Afisa uhamiaji mkoa wa Singida Kamishina msaidizi Bi .Anjela Shija amethibitisha kukamatwa kwa raia hao katika kijiji cha Rungwa tarafa ya Itigi wilayani Manyoni na kusema kuwa walikuwa wakisafirishwa na basi la Sasebosa lenye usajili wa namba T 288 BBM.