Wananchi wamehimizwa kuhifadhi katika mazingira mazuri noti zinazotolewa na Benki ya Tanzania ili ziweze kudumu kwa muda mrefu kwenye mzunguko ili kuipunguzia serikali kuondoka na hasara ya kutengeneza noti mpya badala ya fedha hizo kutumika kwa miradi ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja Msaidizi wa idara ya uhusiano wa benki hiyo, Vicky Msina aliyeko mkoani Kagera,ambapo amesema uchapishaji wa noti unaofanywa mara kwa mara na serikali kuwa unakwamisha mambo mengine makubwa kufanyika