Jumla ya ndoo 54 za samaki wadogo ambazo zimevuliwa kwa kutumia zana haramu katika Bwawa la nyumba ya mungu mkoani Kilimanjaro zimekamatwa wilayani Hai zikisafirishwa kuelekea mkoani Arusha hali ambayo inahatarisha bwawa hilo kufungwa ili kupisha samaki kuzaliana.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bi.Anna Mgwira akiwa na kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya ya Hai amesema pamoja na serikali kupiga marufuku uvuvi haramu katika Bwawa la nyumba ya mungu bado wavuvi wameendelea kukaidi agizo hilo.
Amesema kutokana na tatizo hilo kuna hatari ya bwawa hilo kufungwa ili kupisha samaki wadogo waliobaki kusaliana na kuwataka wananchi wanaozunguka bwawa hilo pamoja na wavuvi kuacha kutumia zana haramu na kufuata sheria kwa kutumia zana zilizoanishwa kuvua samaki wakubwa na siyo samaki wadogo.