Back to top

Afisa wa TRA mtegoni kwa tuhuma za rushwa.

02 August 2019
Share

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU  Imemkamata afisa wa mamlaka ya mapato  nchini  TRA  mkoa wa Ilala bw. Elias Athuman Yunus kwa tuhuma za kuomba rushwa ya dola elfu 17.

Kaimu mkuu wa takukuru  Ilala  bw. Enos  Ngailo  amesema  mtuhumiwa aliomba rushwa kwa mkurugenzi wa  kampuni ya  HEM- HEVY Equipment Company  ltd ili kutoa taarifa za uongo kuhusu  usajili wa mitambo iliyoingizwa nchini kwa lengo la kukwepa kodi.

Amesema uchunguzi wa TAKUKURU  umebaini mtuhumiwa aliomba  milioni  50 na baada ya majadiliano alipunguza hadi milioni 35 ambazo alitaka zilipwe kwa mfumo wa dola za marekani.

Bw. Ngailo samesema mtuhumiwa  alikamatwa baada ya kupokea dola elfu moja.