Matukio ya ukatili wa kijinsia yamedaiwa kuongezeka mkoani Arusha jambo linaloelezwa kuchangiwa na utaratibu wa wadau wengi wa maendeleo kujielekeza kutoa uwezeshaji wa kiuchumi zaidi kuliko uwezeshaji wa kielimu
Kauli hiyo imetolewa na afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha, Bi.Blandina Nkini alipokuwa akizungumza na wadau wanaosaidia kukabiliana na ukatili katika jamii ambao umekuwa ukiwaathiri zaidi wanawake na watoto.