Back to top

Wawili mbaroni kwa tuhuma ya wizi wa transfoma Kagera.

07 March 2020
Share

Jeshi la polisi mkoani Kagera linawashikilia watu wawili wakazi wa mkoa wa Arusha kwa tuhuma ya kuiba transfoma mali ya Shirika la umeme nchini (TANESCO) iliyokuwa imefungwa na shirika hilo katika kijiji cha Kabukome kilichoko katika tarafa ya Rusaunga. 
  
Akisimulia juu ya tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Kamishina Msaidizi Revocatus Malimi amewataja watu wanaoshikiliwa kuwa ni pamoja na Frank Muneja mwenye umri wa miaka 38 na Athumani Sabuni mwenye umri wa miaka 37 ambapo transfoma hiyo ilikuwa imepakiwa kwenye gari aina ya Nissan T.753 DDZ.