Mkuu wa mkoa wa Mara ametishia kufunga soko kuu la Nyasho endapo wananchi watashindwa kuzingatia taratibu zilizowekwa za kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 huku akipunguza muda wa kutoa huduma sokoni hapo ambapo kwa sasa soko litafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na moja jioni tofauti na ilivyozeoeleka.
Mkuu wa mkoa wa Mara Adamu Malima amekuja na uamuzi wakati akifungua kampeni ya kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya corona iliyoandaliwa na Shirika la msalaba mwekundu mkoani na kubaini uwepo wa kiini macho kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wanaweka ndoo za maji na sabuni feki za kunawaia mikono kwenye vibanda vya biashara huku wengine wakileta mzahaa katika kujikinga na maradhi hayo.
Hata hivyo akikagua baadhi ya ndoo zilizokuwa zimewekwa kwenye vibada vya wafanyabiashara mkuu wa mkoa akabaini kibanda ambacho kilikuwa kimekwa maji ya kunawa na sabuni feki.