Back to top

Chanzo cha kifo cha Waziri Mahiga.

01 May 2020
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatangaza kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Balozi Dkt Augustine Philip Mahiga (Mbunge) kilichotokea leo Alfajiri tarehe 01 Mei, 2020.

Mhe.Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma Na amefikishwa hospitali akiwa ameshafariki dunia.

Mhe.Rais Magufuli ametoa salamu za pole kwa familia ya marehemu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai Wabunge,wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria na wananchi wa mkoa wa Iringa kwa kuondokewa ma mpendwa wao,na amesema anaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majozi.

Mhe. Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Balozi Mahiga kuwa alikuwa mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na Mwanadiplomasia mahiri aliyeiwakilisha na kuipigania Tanzania katika nyanja za Kimataifa kwa miaka mingi.