Back to top

Mkutano wa Bunge la 12 la Tanzania waanza leo.

10 November 2020
Share

Mkutano wa 1 wa Bunge la 12 la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  umeanza leo mkoani Dodoma ambapo wabunge wamemchagua mbunge wa jimbo la Kongwa Job Ndugai kuwa Spika wa bunge hilo.

Uchaguzi huo umefanyika chini  ya Uenyekiti wa mbunge wa jimbo la Isimani Willium Lukuvi ambaye aliteuliwa kusimamia kutokana na kuwa mmoja kati ya wabunge wenye uzoefu zaidi ndani ya bunge hilo.

Akitangaza matokeo hayo Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai  amesema Mhe.Ndugai amepata kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa na wabunge hao na hivyo kuwa spika wa Bunge hilo.

Mhe.Ndugai alikuwa Spika katika Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.