Waliokuwa wafanyakazi na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi katika ujenzi wa chuo cha VETA mkoani Geita wameandamana kwenye ofisi ya mbunge wa jimbo la Geita mjini wakiomba awasaidie kulipwa madai ya zaidi ya bilioni moja wanazomdai mkandarasi kampuni ya Sky Ward baada ya serikali kuvunja mkataba na mkandarasi huyo kutokana na kasoro za kiutendaji.
.
Akizungumza na wananchi hao Mbunge wa jimbo la Geita mjini Mh.Costantine Kanyasu ameiomba VETA na wizara ya elimu kuchukua hatua ili wananchi hao wapate haki zao.