Back to top

Mogomo wa Madereva, RC Byakanwa aitisha kikao cha dharura Mtwara.

15 April 2021
Share

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa ameitisha kikao cha dharura cha wakala wanoajiri madereva wa kiwanda cha Dangote, madereva pamoja na uongozi wa Dangote ili kupata muafaka wa madereva waliogoma kufanya kazi kwa siku ya nane sasa wakilalamikia mikataba mibovu ya kazi.  

Mkuu huyo wa mkoa amelazimika kufanya hivyo ili kupata muafaka wa haraka ambao utaondoa mgomo huo ili magari yanayomilikiwa na kiwanda hicho yaweze kusafirisha saruji mikoani ambapo kwa sasa magari yanayopakia saruji ni yale ya watu binafsi.   

Mkuu wa Mkoa Bw.Byakanwa amesema wakati baadhi ya changanoto zikipatiwa majibu katika kikao hicho cha dharura timu ya kufuatilia changamoto zinazokabili madereva hao itaendelea kufanya kazi yake ili kuja na muafaka utakaondoa mgogoro wa mikataba ya kazi baina ya wakala, madereva pamoj na uongozi wa Dangote.

Tume ya siku 21 iliundwa kwa ajili ya kufuatilia changamoto hizo licha ya madereva kugoma wakitaka kuhakikishiwa kwa maandishi maslahi bora na sio kupewa ahadi.