Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amefuta mashamba 11 yenye ukubwa wa Ekari Elfu 24 na 119 na kufufua mashamba 49 yenye ukumbwa wa Ekari zaidi ya Elfu 45 na 788 ambayo yamefutwa hatimiliki yake wilayani Kilosa na kuagiza kugawiwa kwa wananchi ambao hawana mashamba ya kulima.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Wilaya ya Kilosa.
Kwa upande wake Mkuu Wa Mkoa wa Morogoro Bw.Martin Shigela ameishukuru serikali kusikia kilio cha wananchi wa Kilosa.
Wakati huo huo akiwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kimamba Waziri Lukuvi amesikiliza kero zao ambapo kero ya uvamizi wa tembo iligubika mkutano huo.