
Naibu waziri wa Elimu Mhe.Omari Kipanga amesema hatuka kali za kisheria zitachukuliwa kwa wafanyakazi wa sekta ya elimu ambao walihusika na kuvuja kwa mitihani ya sekta ya afya mwaka jana.
Mhe.Kipanga ameeleza hayo Bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa katika wizara hiyo na kubainisha kwamba tayari taratibu za kuanza kuwachukulia hatua watumishi hao zimeanza.
Kabla ya majibu hayo ya Naibu Waziri wa Elimu yalikuja baada ya Mbunge wa jimbo la Songwe Mhe.Philip Mulugo kulalamika bungeni hapo hatua ya Serikali kuwa na ubaguzi katika kutoa adhabu pindi mitihani inapovuja.
Amesema uvujaji huo ukihusisha shule binafsi shule hizo hufungiwa lakini ukihusisha wafanyakazi wa sekta ya umma hakuna hatua zinazochukuliwa.