Back to top

MKUU MPYA WA MAJESHI TANZANIA KUAPISHWA LEO

30 June 2022
Share

Mkuu Mteule wa Majeshi Jacob John Mkunda anatarajiwa kuapishwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania baada ya mtangulizi wake Jenerali Venance Mabeyo kustaafu baada ya kuhudumu kwenye nafasi hiyo kwa Kipindi cha miaka 7.

Mkunda ameteuliwa na Rais Samia Juni 29, 2022, ambapo kabla ya uteuzi huo Mkunda alikuwa Meja Jenerali wa JWTZ.

Mhe.Samia Suluhu Hassan - Rais wa Tanzania.

Wengine wanaotarajiwa kuapishwa leo baada ya kuteuliwa ni pamoja na Meja Jenerali Salum Haji Othman ambaye amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali na kumteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.   
   
Kabla ya uteuzi huo Meja Jenereali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Pia Mwingine aliyeteuliwa anayetarajia kuapishwa leo Juni 30 ni Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Zoezi la la kuwaapisha litafanyika Ikulu ya Dar es Salaam, saa 7 Mchana.