Back to top

WAZIRI MABULA APIGA MARUFUKU UUZAJI WA ARDHI KIHOLELA

01 September 2022
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelina Mabula amepiga marufuku kwa wapimaji na waendelezaji wa Milki kuuza viwanja vyenye vipimo vidogo kinyume cha maadili na atayebaina atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.

Ametoa agizo hilo katika kikao cha wadau wa Ardhi (Milki) mkoani Dar es Salaam ambapo amesema kuwa tokea kuwepo kwa ongezeko la kampuni za uuzaji wa Ardhi kumekuwa na wimbi la uuzaji holela wa maeneo maarufu kama ishirini kwa ishirini ikiwa ni pamoja na kuuza maeneo mara mbili kwa watu tofauti na kuzalisha migogoro baina ya jamii.

Ameeleza kuwa sekta ya aridhi na miliki imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa nyumba bora na gharama nafuu takwimu zilizopo nchini zinaonyesha kuwa kwa mwaka kunatakiwa kujengwa nyumba 200,000 lakini nyumba zilizojengwa ni 13,837.

Dakta Mabula amezitaka taasisi za kifedha hususani Bank nchini kutafuta njia nzuri zaidi ambayo itarahisisha utoaji ww mikopo yenye riba nafuu kwa wananchi katika ujenzi wa nyumba nchini ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo ya urasimishaji wa Ardhi ambapo zoezi hilo litakamilika 2023.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Allan Kijazi amesema sekta Milki inamchango mkubwa katika uchumi wa Taifa lolote lile Duniani lakini kwa Tanzanis bado mchango wake ni mdogo hivyo wameitisha mkutano huo kutathimini sekta ya Ardhi na kuimarisha zaidi mchango wa sekta kiuchumi na kijamii.

Ameongeza kuwa serikali imeanzisha mchakato wa mabadiliko ya sera,sheria na maboresho kimkakati hivyo kupitia mkutano huo wadau wataweza kupata nafasi ya kutoa maoni yao juu ya mabadiliko hayo.