Back to top

Sele Bonge mbaroni kwa tuhuma za uporaji

09 September 2022
Share

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limemkamata Selemani Kalembo (57) maarufu kama Sele Bonge mkazi wa Vingunguti na wenzake 9 kwa tuhuma za kuvamia nyumba na kuiba vitu mbalimbali katika eneo la Kinyerezi, Kibaga mkoani Dar es Salaam ambapo walikamatwa wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba T 218 BYS na vifaa mbalimbali vya kuvunjia nyumba, televisheni 4, kamba na mfuko wa kufichia TV baada ya kuiba.
.
Hata hivyo, Jeshi hilo limebainisha kuwa mahojiano ya kina yanaendelea ili kuwakamata wote wanaoshirikiana nao.