Back to top

MABULA ATAKA UFANYIKE UPEMBUZI MASHAURI YA ARDHI YALIYOKAA MUDA MREFU

07 October 2022
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza ufanyike upembuzi kawa mashauri yote ya ardhi yaliyokaa muda mrefu kutokana na sababu zisizo na mashiko.

Amemtaka Msajili wa Mabara ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stella Tullo kusimamia agizo hilo kwa kumpatia taarifa mapema mwezi Novemba 2022.

Pia amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuangalia kwa jicho la tatu Mabaraza yote ya Ardhi ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya mlundikanao wa kesi za muda mrefu.

Dkt.Mabula alitoa agizo wakati wa Kikao kazi cha Kitengo cha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilichofanyika jijini Dodoma.

Dkt.Mabula amesema, serikali inatambua umuhimu na michango ya mawakili katika kuvisaidia vyombo vya utoaji haki na kuwakumbusha mawakili suala la maadili ya kiutendaj hasa kwa baadhi ya wajumbe kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, uzoefu unaonesha mashauri mengi yanayowakilishwa na mawakili ndiyo yenye muda mrefu kukamilika.