Back to top

Wenye ulemavu Kahama waomba vyumba vya kujifungulia.

13 October 2022
Share

Wanawake wenye ulemavu wilayani Kahama,mkoani Shinyanga, wameiomba serikali itenge vyumba maalum vya kujifungulia  kwenye Vituo vya Afya na Hospitali, wakidai kuwa kundi hilo likichanganywa na wanawake wengine wasio na ulemavu wanapata changamoto , kwani wanahitaji miundombinu na vifaa rafiki .

Wanawake hao wametoa ombi hilo, wakati Mbunge Stella Ikupa, akitoa msaada wa Kitanda cha kujifungulia wanawake wenye ulemavu na vitimwendo vitano, kwa watoto wenye ulemavu, katika Hospitali ya Manispaa Kahama, msaada wenye thamani zaidi ya shilingi  milioni 3.1.