![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/SAMIA_2.jpg?itok=_Ny7yauV)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuanza ujenzi wa Hospitali ya Kanda Mkoani Kigoma, itakayo hudumia mikoa jirani ya Tanzania na nchi za Burundi na Jamhurimya Kidemokrasimya Congo.
Amesema dhamira ya serikali ni kuona Mkoa wa Kigoma unakuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya afya na miundombinu ya barabara na bandari.
Rais Samia ametoa kauli hiyo Oktoba 18, 2022 wakati akiweka jiwe la msingi katika majengo ya wagonjwa mahututi na wagonjwa wa dharura, katika Hospital ya Rufaa Maweni Mjini Kigoma na kuwataka watumishi idara ya Afya kufanya kazi kwa moyo wa kusaidia wananchi.
Katika hatua nyingine Rais Samia mbaye pia alihutubia mamia ya wananchi katika Uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma aliweka jiwe la msingi katika bandari ndogo ya Kibirizi na kuagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuboresha mioundombinu ya barabara inayoingia bandarini hapo.