![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/2022.jpg?itok=F-PMnPDz)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa Tanzania ina Jumla ya idadi ya watu ni mil .61,741,120
Rais Samia ameeleza hayo wakati akishiriki uzinduzi rasmi wa matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, iliyofanyika Jijini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa Tanzania Bara ina idadi ya watu 59,851,357 na Tanzania Zanzibar ina idadi ya watu 1,889,773.
Pia Rais Samia amebainisha kuwa, kutokana na matokeo hayo ya Sensa ya mwaka 2022, Idadi ya wanawake ni milioni 31,687,990 sawa na 51% na wanaume ni milioni 30,053,130 sawa na 49%.
Rais Samia amesema katika kipindi cha miaka 10 kuna ongezeko la watu milioni 16.8 sawa na asilimia 3.2.
Kwenye matokeo ya Sensa ya 2022, yameonesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ndio unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu nchini ambao ni milioni 5.3 sawa na asilimia saba na kufuatiwa na Mwanza watu milioni 3.6 sawa na asilimia sita.
Miaka kumi iliyopita Tanzania ilikuwa na watu 44, 928, 923 hii inaonyesha kumekuwapi na ongezeko la watu milioni 16,812,197 sawa na ongezeko la asilimia 3.2 ya waliokuwepo kati ya mwaka 2012 na mwaka 2022.