Back to top

MAKALLA ATANGAZA KUSITISHA MGAO WA MAJI DAR ES SALAAM.

25 November 2022
Share

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Amos Makala, ametangaza kusitisha mgao wa maji Mkoa wa Dar es Salaam.

Hatua hiyo imekuja baada ya kutembele mitambo ya Ruvu Chini iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani na kujiridhisha mto huo kuanza kujaa kufuatia mvua zilizoanza kunyesha kwenye baadhi ya mikoa ikiwemo Mkoa wa Morogoro.

Akizungumza baada ya kutembelea mitambo hiyo ya maji Ruvu Chini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Amos Makalla, amesema pamoja na kusitishwa mgao wa maji, watumiaji wa maji waendelee kutumia maji kwa ungalifu.

Makalla ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, kusimamia vyema miundombinu inayotengenezwa na mamlaka hiyo Mkoa wa Dar es Salaam ili kuondoa hali ya ukosefu wa upatikanaji wa maji kwa wanachi.