Back to top

Kapembe afariki dunia akishuka Mlima kilimanjaro.

14 December 2022
Share

Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mkoani Manyara, Joachim Kapembe, amefariki dunia alipokuwa akishuka kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Kapembe pamoja na watendaji wengine wa wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari walipanda kwenye Mlima Kilimanjaro, tarehe 9 mwezi huu, kwa ajili uzinduzi wa intaneti ya mwendokasi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).


Marehemu ameacha  mke na watoto wawili.