Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesitisha shughuli za Bunge, baada ya kutokea kwa hitilafu katika mfumo wa sauti.
.
Hali hiyo imejitokeza baada ya vinasa sauti na vipaza sauti katika Jengo la Bunge kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha ambapo sauti ilikuwa ikikatikatika.
.
Hata hivyo mafundi wanaendelea na matengenezo ya mfumo huo, huku shughuli za Bunge zikitarajiwa kuendelea baada ya nusu saa.