![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/JAAA.jpg?itok=6z0PhnnO)
Serikali imesema imeweka kipaumbele katika kuimarisha huduma za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema kupitia mifumo, Sera na Teknolojia.
Taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Jafo, amesema hayo wakati akizungumza kwenye Jukwaa la Mawaziri la Majadiliano ya Juu la Utekelezaji wa Tahadhari ya Mapema kwa Wote katika Mpango Kazi wa Afrika lililofanyika pembeni ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Dkt.Jafo amesema serikali inahakisha inapunguza athari za majanga kwa kuboresha ustawi na uthabiti wa watu wake na jamii kama sehemu ya mkakati wa maendeleo kwani majanga matokeo ya maafa yanaathiri mipango na malengo ya maendeleo yake.
Amesema kutokana na taarifa za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa, serikali na wadau wote wenye dhamana imeandaa Mpango wa Taifa wa Dharura wa El Nino na hatua ya matarajio Agosti, 2023 ambao umechangia kupunguza athari za mvua hizo.