Matumaini ya Mchezaji wa Kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, yameanza kurejea baada ya kifungo chake cha miaka minne kwa kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli kupunguzwa hadi miezi 18, kufuatia rufaa iliyofanikiwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas).
Vyanzo vilivyo karibu na kiungo huyo wa kati wa Juventus, mwenye umri wa miaka 31 viliiambia shirika la 'BBC Sport' kwamba, mchezaji huyo anaweza kuanza mazoezi tena Januari 2025, na atastahili kucheza tena kuanzia Machi.
Pogba alisimamishwa na mahakama ya kitaifa ya Italia ya kupambana na dawa za kusisimua misuli (Nado), mwezi Februari, baada ya uchunguzi wa dawa kubaini viwango vya juu vya testosterone - homoni katika mfumo wake ambayo inachochea kusisimua misuli.