Back to top

19 wajeruhiwa ajali ya Lori na Daladala Mwandege Mkuranga Mkoani Pwani

08 March 2020
Share

Watu 19 wamejeruhiwa baada ya Lori la Mchanga na Daladala kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Mwandege Mkuranga Mkoani Pwani, ambapo wanaume ni 15 na wanawake 4.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesmo Lyanga amesema majeruhi wanapatiwa matibabu hospitali ya Temeke Zakiem Mbagala jijini Dar es Salaam huku akisema wanachunguza chanzo cha ajali kisha watakitolea majibu.

Kamanda wa Polisi Lyanga ameongeza kuwa dereva wa Lori la Mchanga lililokuwa likielekea Mkuranga na dereva wa daladala linalofanya safari zake Temeke kuelekea Kisemvule wanapatiwa matibau hivyo afya zao zikiimarika wataweza kuzungumza nao ili kujua chanzo cha ajali. 

Hata hivyo hivyo mashuhuda waliokuwa katika eneo hilo wao wamesema chanzo cha ajali ni dereva wa daladala aliyekuwa akijaribu kulipita Lori hilo la mchanga ndipo akaangukia pembezoni mwa msitu wa hifadhi ya Vikindu.