Back to top

BAADA YA AJALI, SAFARI ZA PRECISION AIR ZAANZA TENA BUKOBA

11 November 2022
Share

Kampuni ya ndege ya Precision Air, iliyositisha safari zake kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba, baada ya moja ya ndege ya kampuni hiyo kupata ajali na kusababisha vifo vya watu 19 na kuwajeruhi wengine 24, baada ya kutumbukia ndani ya maji ya Ziwa Victoria leo imezindua tena safari zake katika uwanja huo.

Moja ya ndege ya kampuni hiyo imetua kwenye uwanja wa Bukoba majira ya Alasiri ikiwa na abiria 23 ambao baadhi yao wamesema kuwa safari hiyo ilikuwa nzuri na kueleza kwamba hawakuwa na hofu na kitu chochote walipokuwa angani.

Baadhi ya watoa huduma katika uwanja huo wakiwemo madereva wa taxi, wamesema ajali ya ndege hiyo iliwaathiri sana kwa sababu uwanja ulifungwa hivyo wamepongeza serikali kufungua uwanja wa Ndege wa Bukoba na uamzi kampuni ya Precision Air. kuanza safari zake tena katika uwanja huo.