Back to top

BASSIROU FAYE AAPISHWA KUWA RAIS WA SENEGAL

02 April 2024
Share

Bassirou Diomaye Faye, ameapishwa kuwa Rais wa Tano wa Senegal ambapo ameahidi kufanya mabadiliko ya kimfumo, uhuru pamoja na utulivu kwenye nchi hiyo.
.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 44, ambaye anakuwa Rais kijana zaidi kuwahi kuliongoza taifa hilo, na kwamba anachukua nafasi hiyo huku kukiwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira, hasa kwa vijana ambao ni karibu 75% katika nchi hiyo yenye watu milioni 18. 


Ikumbukwe Faye, baada ya kutangazwa mshindi alisema vipaumbele vyake ni maridhiano ya kitaifa, kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha na kupambana na ufisadi.