Back to top

SHINYANGA MKOA WA NNE KWA MAAMBUKIZI YA MALARIA

12 December 2024
Share

Mkoa wa Shinyanga umebainishwa kuwa mkoa wa nne, ukiwa na asilimia 16 katika mikoa mitano inayoongoza kwa maambukizi makubwa ya vimelea vya Malaria.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga, Bi.Bety Shayo katika kikao kazi cha uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria inayotekelezwa chini ya Wizara ya Afya, Tawala za Mikoa na Serikalim za Mitaa na Bohari Kuu ya Dawa, kwa ufadhili wa Global Fund, ambapo vyandarua zaidi ya Milioni Moja na Laki tano vitagawiwa kwa wakazi wa mkoa huo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bw.Timothy Sosoma amesema Idara ya Afya ya mkoa huo, imejipanga kuhakikisha kila Kaya inapata vyandarua kulingana na idadi ya watu.

Afisa Mradi wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria , Wizara ya  A fya, Bw.Wilfred Mwafungo amesema malengo ya Serikali ni kuhakikisha miaka ijayo Tanzania inafikia kiwango cha malaria asilimia sifuri au Digiti moja.