Back to top

Bugando kuazisha kliniki ya Madaktari bingwa wa jioni

09 August 2018
Share

Zaidi ya Madaktari 50 katika hospitali ya rufaa Bugando mkoani Mwanza wanataraji kushiriki katika zoezi la utoaji matibabu ya jioni yatakayo kuwa yanatolewa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za kibingwa kutoka kwa madaktari bingwa.

Mkuu wa idara ya magonjwa ya ngozi katika hosptali hiyo Dokta Norasco Mang'ondi amesema mpaka sasa wanahudumia zaidi ya wagonjwa 2000 kwa mwezi kupitia huduma za bima za afya na malipo ya papo kwa papo.

Nimekuwekea VIDEO kuona taarifa hiyo na nyingine zilizoruka kwenye habari za saa.