DAR ES SALAAM.
Wanafunzi watatu wamefariki dunia baada ya Moto uliozuka usiku wa kuamkia leo kuunguza bweni la shule ya sekondari ya Ilala Islamic iliyopo eneo la mtaa wa Arusha Ilala.
Mpaka sasa chanzo Cha Moto huo hakijajulikana ambapo wanafunzi wote wa shule hiyo wamehamishiwa kwenye shule ya msingi ya Ilala Islamic iliyopo jirani na eneo hilo kwa ajili ya kupatiwa hifadhi wakati taratibu zingine zikiendelea.
Aidha jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama imefika katika eneo hilo ambapo sasa inaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha moto huo.
Shule hiyo ya sekondari ya Ilala Islamic ina takribani wanafunzi 350 wa kutwa na bweni ambapo wengine waliokuwa bwenini walifanikiwa kujiokoa.
Endelea kufuatilia taarifa zetu kufahamu zaidi.