Waziri wa Ujenzi Mh. Innocent Bashungwa amesema Wizara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), inatarajia kuanza kutekeleza mradi wa kimkakati wa Ujenzi wa Daraja la Jangwani ili kutatua changamoto ya kujaa kwa maji katika barabara ya Dar es Salaam-Morogoro, wakati wa mvua na kusababisha kufungwa kwa barabara hiyo.
Bashungwa ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa Fedha 2024/25.
Amesema mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maendelezo ya Bonde la Mto Msimbazi.
Bashungwa amesema daraja hilo litakalojengwa lina urefu wa mita 390 pamoja na Barabara unganishi zenye urefu wa mita 710 na kina cha mita 15.5 kutoka usawa wa bahari.