Back to top

DART: ABIRIA WALIMUAMRISHA DEREVA KWENDA KIMARA

28 March 2024
Share

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema vurugu kati ya abiria na madereva wa basi liendalo haraka uliotokea mnamo Machi 26, 2023, saa mbili usiku katika eneo la Kivukoni, ulitokana na abiria wengi waliokuwa wanasubiria basi la kwenda Kimara kwa muda kuamua kuingia kwenye basi hilo la Morocco lililokuwa Kituoni kupakia abiria wa Morroco na kumuamrisha dereva wa basi hilo akiwa na mwezake kuwapeleka Kimara.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Wakala huo umeeleza kuwa madereva hao waliendelea kusimamia ratiba ya basi na kukataa kuwapeleka abiria hao Kimara na madereva hao kupeleka basi Morroco, na baada ya malumbano ya muda mrefu madereva wakaamua kuwarudisha abiria hao Kivukoni kitu ambacho DART imesema sio busara, na kwamba malumbano yalipozidi ndipo walipoamua kuwapeleka abiria hao Kimara. 
.
Kufuatia sintofahamu hiyo DART imewasimamisha kazi watumishi wawili ambao ni Shabani Kajiru - Msimamizi wa Kituo cha Kivukoni na Brown Mlawa - Afisa Ufuatiliaji wa Kituo, ili kupisha uchunguzi.