Makandarasi nchini wameaswa kufanya kazi kwa weledi ikiwemo kufanya kazi kwa kutumia wataalam, ili kufanya miradi yenye tija iliyokusudiwa kulingana na mikataba wanayoingia na waajiri wao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe.Saad Mtambule, wakati akihitimisha mkutano wa mashaurino na wadau wa sekta ya ujenzi iliyofanyika mkoani Dar es Salaam na kukutanisha wadau wa ujenzi kutoka mikoa ya Kanda ya Mashariki.
Mwenyekiti wa bodi ya CRB Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema mikutano hiyo iliyoandaliwa na bodi ya wahandisi kwa mikoa ya Mwanza,Mbeya,Arusha na Dodoma imekuwa ya manufaa kwa sekta ya ujenzi nchini kutokana na Makandarsi kuweka maazimio ya pamoja.
Mkutano huo umekutanisha washiriki 592 ambapo washiriki 527 ni Makandarasi huku washiriki 65 wakiwa ni wadau wa sekta ya ujenzi,pia mkutano huo umeenda sambamba na maonesho teknolojia, huduma na vifaa vya sekta ya ujenzi.