Back to top

'Dhamana ya Mbowe na Matiko wa CHADEMA bado ngoma nzito'

28 November 2018
Share

Jaji Samu Rumanyika wa Mahakama Kuu ya Dar es Salaam muda mfupi uliopita amesimamisha kusikiliza kesi ya maombi ya dhamana inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbunge wa Hai Mh. Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini Mh.Esther Matiko na kuagiza karani wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupeleka jalada la mwenendo mzima wa uamuzi wa kufutwa kwa dhamana ya viongozi hao na ndipo aendelee kusikiliza na kutoa umuazi juu maombi ya rufaa ya dhamana ya vongozi hao waandamizi wa Chadema.

Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na baadhi ya wanachama vyama vya upinzani nchini wamejitokeza kwa wingi katika mahakama kuu jijini dar es salaam kwa ajili ya kusikiliza maombi yaliyowasilishwa mahakamani kuu na wakili Peter Kibatala.